Monday, May 18, 2015

WANANCHI WA SONGEA WAPEWA ELIMU YA UPANDAJI WA MAHINDI KWA NJIA BORA

Mtaalamu wa kilimo kutoka Rubuye Agrobusiness Co. Ltd Bwana Boniface(Wa pili kushoto) akiwaonyesha wakulima wa mahindi wa Songea Vijijini namna mahindi yanavyoweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali hivyo kuwapa mbinu ya namna ya kukabiliana na changamoto hiyo ili kuweza kujiongezea kipato kwa kuzalisha mazao mengi na yenye ubora.

Bwana Boniface Manga(Wa kwanza Kulia) ambaye ni mtaalamu wa kilimo kutoka Rubuye Agrobusiness Co.Ltd akiwaelekeza wakulima wa Wilaya ya Songea Vijijini njia sahihi za kufuata wakati wa kupalilia mahindi ili kuepuka kukata mizizi itakayosabaabisha kudumaa kwa mahindi na kushindwa kutoa mazao bora.

No comments:

Post a Comment