|
Wanafunzi wa shule ya msingi Usetule wakishusha mifuko ya Cement waliyokabidhiwa na kampuni ya Rubuye Agrobusiness Ltd. |
Na: Naverine Mgeni
Ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanakuwa na ufaulu mzuri kampuni ya Rubuye Agrobusiness Ltd iliamua kuchangia mifuko ya Cement 20 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Usetule iliyopo katika halmashauri ya Mji wa Makambako.
Hii ni moja ya shughuli za kijamii ambazo zimekuwa zikifanywa na kampuni kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii ambao mara zote ndio wamekuwa na mchango mkubwa kwa kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Mkoa wa Njombe hususani watu wa Makambako wamekuwa wakitegemea kilimo kama ndio kazi mama ambayo imekuwa ikitoa ajira kwa wengi.